JOBLIZ

  • Latest News

    JINSI YA KUMSHUGULIKIA MTU AKUSEMAYE VIBAYA AU MWENYE ROHO MBAYA

    Mtu mwenye Roho mbaya ana majina mengi na ana nazo sifa nyingi zinazo mtambulisha na wanapatikana katika kila nyanja ya maisha. Toka kwa Mtoto mdogo hadi mkongwe ,Msomi na hata asiye msomi  muumini wa Dini na kwa wapagani pia.Wao sifa zao kubwa ni kuzungumza ya watu na kulaumu wengine kuwa wana makosa. Watu wa jinsi hupenda kuua ujasiri wako kwa kukulaumu hata kwa matendo ambayo hukufanya au umefanya lakini ilikuwa sio kwa nia mbaya.Hupenda kubadili habari njema yako kuwa mbaya hubadilisha  mtazamo wako .Mara nyingi husababisha wewe uwe na msongo wa Mawazo na Afya Mbaya.watu wa jinsi hii huyafanya maisha yako kuwa ya Mashaka na upweke.Masengenyo  yao na ubaya wao huusambaza ili maisha yako yaharibikiwe na uonekane duni katika jamii na Ndugu zako.
    Kuwa shughulikia watu wa jinsi hii huwa ni ngumu na hasa wale wenye tabia ya kulaumu na kusambaza lawama kwa Jamii .Ndugu na rafiki zako.Mara nyingi jambo baya likitokea katika jamii mara nyingi kulielekeza kwa wengine iliwao wasionekane wabaya kwa kukusukumia lawama.Kuwashughulikia watu wa Jinsi hii mara nyingi hukuacha uwe na Msongo wa mawazo na kuwa na Afya mbaya .Ushauri mzuri ni kuwapuuza na kuwatoa katika mzunguko wa maisha yako.Sio rahisi kuwatambua watu wenye tabia mbaya kirahisi kwakuwa wanakuja katika kila aina ya Maisha ya Binadamu.Nita kwenda kujadili sifa chache ambazo zita mtambulisha mtu mwenye Roho mbaya na Baadae nitatoa njia ya jinsi ya Kuepukana nao .

    SIFA ZA DALILI ZA MTU MBAYA 
    1Mtu mbaya huwa hakubali kuwa amefanya kosa hata kama amekosea atatafuta njia ya kuipeleka lawama kwa mwingine au atatengeneza kila njia kuhakikisha anamkoseha mwingine kwa kumshauri vibaya au kumshawishi atende jambo baya ililile kosa alilofanya yeye lihamie kwa mwingine aionekane yeye kuwa amehusika na kosa hilo.Na hawa ombi msamaha kokote kwakuwa wao wanajiona kuwa hawana hatia.
    Na hata wakiomba msamaha huwa ni wa kinafiki bado wakikurudishia lawama kwako kwamba kama usingelikuwa wewe wasingalikosea hivyo ni kwa makosa yako ndiyo maana wamekosea.Mara nyingi watu kama hawa  hupata sifa yakufanya vizuri kama tatizo likiisha vizuri na wewe kuonekana kama hufai mbele za wengine yeye akiwa ana faa zaidi yako.
    2.Mtu mbaya kukataa hata kama amefanya kitu kibaya hakubaki kuwa amekifanya yeye hata kama unaushahidi wa kutosha atakataa na aatsema kuwa wewe ni mwongo atabisha kwa kuwa watu kama hao huwa hawayakubali makosa  yao.Hata kama wanajua kuwa wamekosea mtu mbaya atendelea kubisha tu iliaonekane kuwa hana hatia hata kama anayo hatia ya kosa alilolifanya na ushahidi upo lakini ataendelea kubisha na kutafuta namna ambayo aonekane ni mwema na wewe ni mbaya.
    3Mtu muovu hushangilia na kuyatangaza mambo yako kwa wengine haraka sana anapokugundua umefanya makosa .sababu kubwa ili yeye aonekane kuwa ni mwema kwa jamii na ndugu wewe ni mbaya sana .Watu wabaya hujitahidi sana kukupiga majungu iliusifanikiwe na hasa wakiona umepata fursa ambayo wao pia wanaweza kuipata hujitahidi sana kutapakaza uvumi wa uongo haraka sana iliiwezekusikika na kwa uovu wao wata kusema vibaya ili ukate taama usifanikishe katika fursa iliyojitokeza ili wao waichukue fursa hiyo.
    4Bahati mbaya sana watu wabaya huwa  hawajitambui kuwa ni wa baya kiasi gani.Na huwa hawa sikii maumivu au hisia ya uchungu wanayokufanyia.Na hata wakijua kuwa umetambua uovu wao watakuambia nilikuwa na kutania tu maana wao wema kwao kumetiwa ganzi na wanafurahia kukuumiza kwa maneno au kwa maandishi yao.Hufurahi kukukebehi wakiwa wanajua kuwa wana kuumiza wao  haiingii Akilini mwao kuwa wanatenda lakukuumiza kwakuwa wanafurahia kuumia kwako..
    5Watu wabaya Wanaamini kuwa mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Matakwa yao na mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Hupenda sana kuutumia mgongo wako kuficha uovu wao iliwao wapate na wewe ubebe lawama zao.
    6.Tabia nyingine mbaya ya watu hao ukijihami kutokana na tamia mbaya yao watakuzulia jambo na kulitangaza vibaya iliuonekane wewe ni mbaya na hufai katika familiana ukoo au jamii uliyonayo
    7.Hawapendi mabadiliko ya maendeleo yako haswa ikiwa kwamba wao watakuwa wamepata kulingana nao wewe  kuwazidi wao wata chukia u wanapenda wao ndio wa miliki sehemu kubwa kukushinda wewe au sehemu nzuri zaidi ya wewe waonekane wao wako juu zaidi yako .Hawapendi wewe upate heshima sawa na wao au kuwazidi lakini wao tuu ndio wawe na heshima na kupendwa zaidi ya wewe.
    8.Watu wao hawana chema cha kusema kwako mara nyingi ni kukulaumu na kukubeza hata kama uwafanyie jema gani lazima waweke sababu ya wao kujikweza iliuonekane hata kile chema ulicho kifanya bila wao usingalikifanya hivyo wao ndio wanaostahili heshima na kuaminiwa na sio wewe .

    JINSI YA KUPAMBANA NA MTU MUOVU NA WANAFIKI

    Baada ya kusaka mbinu mbalimbali kwenye mtandao na majalida mbalimbali ya kisaikolojia hakuna njia nzuri katika kupambana na mtu muovu mnafiki na mbaya zaidi ya wewe mwenyewe kwanza kujikubali kujiamini kuwa wewe unaweza na lawama zao ni za kijinga na za kitoto na wewe ni mtu mkubwa usiyeyumbishwa na mambo ya kijinga pia yapo mambo ya msingi ya kufuata kama ifuatavyo.
    1Kubali kwanza binafsu kuwa wewe hutaweza kuwa badilisha tabia zao kwakua hata kubali makosa yao na hawata kuomba msamaha kwa makosa waliyokutendea wala hawata jirekebisha na tabia ya kukuumiza wewe.Hivyo jikubali mwenye usiishi kwa kuwategemea wao maisha yako.Hata ujitahidi namna gani hauta waridhisha katika jitihada zako.kujitahidi kufanya vizuri kwao hakutakusaidia kuwa fanya wao wasikuseme vibaya.Inakupasa uachilie moyoni mwako kuwa wanapaswa uwaondoe maishani mwako iliuweze kusonga mbele na maisha yako vizuri maana huta pata muda wa kuvisikia au kuwasikia maneno maovu juu yako.
    2.Usichukue muda wako kujitetea na kujihami katika maneneo yao kadri unavyojitetea ndivyo maneno mabaya yanavyo tapakaa juu yako hivyo ni vema kukaa kimya na kuchunguza iwapo kuna jambo baya ulikosea kweli ni kurekebisha tabia hiyo mbaya na kusonga mbele na maisha yako.Kama wamekulaumu kwa kukusingizia jaribu kujieleza kuonyesha jinsi gani huhusikia na usijaribu kujitetea wacha waamue wao wewe songa mbele na maisha yako.
    3.Usitunze dhihaka zao wanazo kukejeli nazo mf.Utakufa masikini.Huna akili wewe ya maisha wewe si mjanja wa maisha ni mbumbubu .Una watoto wengi hivyo umeyakosa maisha. Mara nyingi kejeli kama hizi wanazaokufanyia watu waovu huwa hawana majibu ya kukusaidia wewe isipokuwa ni kukubeza tu .Wazo la mtu moja kwako la kukubeza haliwezi kuwa ndio ukweli wa maisha yako.Huwezi kuendelea kuishi katika maisha yako yote ukiwa muathirika wa mioyo yao miovu inakupasa ujiamini na kuanza kuishi maisha yako.
    4.Kujiamini ni ufunguo baada ya kuumizwa sana na kwa maneno na watu waovu wasio na masaada kwako.Jipe ujasiri usiamni yote unayolaumiwa nayo na watu waovu.Mara nyingi mbegu ovu iliyopandwa na mtu muovu huacha maumivu kwenye nafsi jiamini itakutoa katika mitego ya watu waovu na watakuheshimu baada ya wao kukosa meneo ya kutaka kukulaumu.
    5.Usifanye malumbano na mtu muovu kwakuwa mantiki unayotaka kufanya haipo nafsini mwake isipokuwa ni kukulaumu na kukoona ni mkosaji mara zote.jambo la msing acha malumbano na mtu muovu matokeo yake atakumiza nafsi bure.
    6.Punguza au acha kuwa na mahusiano nao na kama ikishindikana jitahidi kuwepo na shahidi kati yenu na hasa kama kuna mgogoro kati yenu kama hayupo shahidi jitahidi kuepakana naye katika mijadala yeyote  naye.
    7.Usionyeshe kuumizwa na neno lolote baya walio kufanyia hata kama wamekumiza usijionyeshe kuwa wamekuumiza au wa mekupata katika kusudio lao baya.Usikichukulie kila kitu wasemacho katika uhalisia na wao wakakusoma kwa hilo wamekupata uwe shujaa na Moyo wenye ulekevu.
    8.Uwe na mpango mbadala B mf.iwapo umekwenda nao sehemu wewe huna usafiri binafsi usi wategemee asilimia mia kuwa watakurudisha pale ulipotarajia kufikia.au ulikuwa na jambo umewaomba msaada wakusaidie watu  wabaya sio wakutegemea kuwa watakusidia kutatua tatizo lolote lilikufika uwe na Mpango Mbadala wa matatizo yako hao sio wema wenzio ni nyoka kwa matatizo yako watatafuta sifa na kukubeza nakuijiona wao wanafaa sio wewe utabaki na lawama tu kuwa wao wamtumia hiki na kile kukusaidia wewe mshindwa.
    9.Weka mpaka kati yako na wao uwe ni mpaka wa kihalisia au wa kimawazo wekafikira kuwa lawama zao zote hazikufikii na hazikuumizi mawazo yako.Dhibiti mipaka yako na hakikisha hawavuki kuja kukudhuru wewe kifikira katika maisha yako haijalishi ni tatizo lipi hakikisha huwapi mwanya wa kuwapa nafsi ya kupenyeza laumu zao
    10 Usiwape nafasi wakubadili msimamo wako wasikufanye usononeke kwa lawama zao Matatizo yako sio makosa yako na wala sio makosa yao.Tambua mahitaji yako na kile kitu unachokihitaji fanya kile unachokiamini.fanya maamuzi mazuri katika maisha yako tengeneza maisha yako kwa kufanya maamuzi mazuri sahihi.Jitahidi kutatua kila tatizo la kimaisha  hakikisha kuwa hakuna anayekulaumu kwa kufanya yale unayoweza kuya mudu usifanye mashindano kwa yale usiyoyaweza kwa kuogopa kulaumiwa weka msimamo wako wa yale yaliyo ya haki tu.
    11.Usipende kutoa ushauri kwa mtu lawama kwakuwa lisipofanikiwa itakuwa umempa nafsi mtu muovu kupenyeza mambo yake kukuona hufai na ushuri wako sio mzuri.Watakapo kujakukuomba ushauri wakumbushe kwa shauri liloshindikana hapo mwanzo iliusiangukie kwenye mtego wa mwanzo tena usibishane na mjinga kwakuwa watakuvuta katika hatua ambayo watakuangusha.Mbinu nzuri jinsi ya kupambana na mtu lawama na mnafiki ni kubadili mwelekeo wako wa Maisha jitahidi kuwa na msimamo usio yumbishwa kirahisi na kuingizwa kwenye mtego wa kulaumiwa na kuonekana hufai katika Maisha haya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    2 comments:

    Item Reviewed: JINSI YA KUMSHUGULIKIA MTU AKUSEMAYE VIBAYA AU MWENYE ROHO MBAYA Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top