JOBLIZ

  • Latest News

    MPINGA KRISTO HUYU HAPA

    Kulingana na Maandiko mpinga Kristo ni mtu yoyote anayepinga kuwa YESU NI MWANA WA MUNGU Aliyekuja katika mwili na kufa msalabani kwa ajili ya kuwa komboa watu.
    /Wote tunajua kuwa Dini zote zisizo za kikristio zikiwemo Uislamu,Mabudha,Mayahudi,Wahindu hizi zote ni dini wapinga kristo kwa imani ya kikristo.Je vipi kuhusu dini za kikiristo?
    Ni jambo la kushangaza sana kuwa kuna madhehebu mengi sana sasa ya Kikirstu yana upinga ukweli huu ya kuwa YESU Kristo ni MWANA WA MUNGU ya kuwa alitumwa na MUNGU BABA katika Roho Mtakatifu akazaliwa na Bikra Maria katika Mwili.Ukweli ni kwamba madhehebu mengi hayo ya Kikristo yana amini kuwa YESU KRISTO ni MWANA WA MUNGU kihalisia yale wanayosema na Bibilia inavyothibitisha ni vitu viwili tofauti.
     1.Yohana 4;9Katika hili pendo la Mungu kwetu, Kwamba Mungu amemtuma  Mwanae pekee ulimwengu upate uzima kwa yeye
     Hii ni kudhibtisha kuwa ni kweli Mungu alimtuma Mwanae wa pekee aukombomboe Ulimwengu hivyo huu ni ukweli kuwa Mungu alikuwa na Mwana kabla ya kumtuma kuja kuzaliwa na Bikira Mariam.Hivyo kama angalikuwa hana Mwana asingaliweza kumtuma kuja hii ina dhibitisha Yesu Kristo alikuwepo hapo Mwanzo kabla hajazaliwa na Bikra Mariamu. ina thibitishwa na Andiko hili.
    Yohana 17;5 Na sasa Baba,Unitukuze mimi pamoja nawe ,pamoja nawe ,kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
    Andiko hili linadhibitisha kuwa Yesu Kristo alikuwepo kabla ya Ulimwengu kuwako .Hii inathibitisha kuwa kulikuwapo MUNGU BABA NA MUNGU MWANA wakiishi pamoja katika Utukufu.Hii ni kudhibitisha ROHO MTAKATIFU MUNGU BABA alimzaa ROHO MTAKATIFU MUNGU MWANA kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote na kwa kwa kupitia MUNGU MWANA kila kitu kiliumbwa kupitia YEYE.
    Yohana 1.3Vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika kitu chochote kilichofanyika.
    Nakushauri kwa nguvu kuwa USOME BIBILIA iliuweze kuujua ukweli huu wa MUNGU.
    Kuzaliwa Kwa Yesu katika Roho Mtakatifu ulikuwepo kabla ya Misingi  ya Ulimwengu huu kuwepo hapo Mwanzo.
    Yohana 1;1-3 Hapo mwanzo kulikuwepo na NENO naye NENO alikuwapo kwa MUNGU ,naye NENO alikuwa kwa MUNGU .2Huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU .3Vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika kitu chochote kilichofanyika.
    TAFADHALI ielewe Bibilia kuwa haiwezi kusema huwa hapo Mwanzo kulikuwapo MUNGU BABA kwa kuwa MUNGU BABA hana mwanzo lakini MUNGU MWANA anao Mwanzo ambapo MUNGU BABA alimzaa MUNGU MWANA
    Katika Yohana 1;1 ina sema Naye Neno alikuwa MUNGU . YESU ni MUNGU kwakuwa ni MUNGU MWANA yeye ni wa ELOHIMU MUNGU BABA.YESU MUNGU MWANA (YESHUAH)ambaye si sawa na (YAHWEH)ambao wapo ni Mungu Baba Na Mungu Mwana Nafsi Mbili.Ambapo Mungu Baba ni Mkuu kuliko Mwana kama inavyo thibitishwa kwa maandiko mengi
    1.Marko 16;19 Basi Bwana Yesu ,baada ya kuyasema hayo yote akachukuliwa juu mbinguni akaketi mkono wa kuume wa Mungu .
    2.Wakolosai 1;Kwakuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa ,vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,vinavyoonekana na visvyoonekana;ikiwa ni viti vya enzi ,au usulutani,au enzi ,au mamlaka,;vitu vyote viliumbwa kwa njia yake,na kwa ajili yake.
    3.1 Wakorintho 11;3 Lakini nataka mjue ya kuwa kila kichwa cha mwanaume ni Kristo,na Kichwa cha mwanamke ni mwanaume,na kichwa cha Kristo ni MUNGU.
    4.Yohana 14;28 Mlisikia kuwa mimi niliwaambia ,naenda zangu ,tena naja kwenu,.Kama mngalinipenda,mngalifurahi kwa sababu nakwenda kwa Baba ;kwa maana Baba ni Mkuu kuliko Mimi.
    Yesu anafana sawa Na Baba yake Yesu ni Roho hakuumbwa mtakatifu wa milele aliyemkamilifu na wa kweli aliye chini ya Mamlaka ya Baba yake.Kuzaliwa na sio kuumbwa ambaye huumtii Mungu Baba Katika kila kitu na mtumishi mwaminifu kwake.aliyehusika katika uumbaji.
    Wakolosai 1;15 Naye ni Mfano wa MUNGU asiye onekana ,mzaliwa wa kwanza katika viumbe vyote.
    Kwahiyo Yesuah Elohim ni mzaliwa wa kwanza wa Yahweh Elohim amepewa Mamlaka ya vitu vyote vilivyoko Mbinguni na vilivyoko juu ya nchi
    Waebrania 1;6 Hata amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni ,asema na wamsujudu Malaika wote wa MUNGU
    Madhehebu mengi ya Dini ya kikristo yameukosa ukweli huu wa kuzaliwa kwa Yesu kiroho na yamendelea kuishi katika Giza la kiimani.Kuzaliwa Yesu katika Roho ndio msingi mkuu wa imani .Kupinga kuzaliwa kwa Yesu katika Roho ni kupinga uhalisia kuwa Mwana wa Mungu alikuja Kwa Roho na Kuzaliwa Mariam kuvaa mwili.
    Neno Mpinga Kristo limetajwa mara nne katika Bibilia na yote na Mtume Yohana katika Nyaraka zake .
    1.Yohana 2.18 Watoto,ni wakati wa mwisho;na kama mlivyosikia kwamba  mpinga Kristo yuaja,hata sasa wapinga kristo wengi wamekwisha kuwepo,kwa sababu hiyo twa jua kuwa  ni wakati wa mwisho.
    1.Yohana 2;22 Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo?Huyo ndiye mpinga Kristo,yeye amkanaye Baba na Mwana.
    1Yohana 4;3Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu.Na hii ndiyo roho ya mpinga kristo ambayo mumeisikia kuwa yaja ;na sasa imeshakuweko duniani.
    2.Yohana 1;7 kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani ,wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili .Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
     Hivyo mpinga kristo ni yule anayekana kuwa Yesu ni Kristo na kuwa Ni MUNGU mwana aliyezaliwa na MUNGU Baba akaviumba vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi na kutumwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akazliwa na Bikira Mariamu akauvaa mwili.
    Madhehebu mengi ya kikristo yana ukana ukweli huu na yakiamini kuwa Yesu alikuwa ni Malaika kabla ya kutumwa duniani ni Uongo mfano wa madhehebu hayo ni Mashahidi wa Yehova,Madhehebu ya dini asilia ya dini za kikristi,kanisa la Unitarian, orthodox na kadhalika.
     Yesu Kristo alipomaliza kazi na kuikamilisha vizuru pale msalabani alirudi katika Utukufu wake Katika Mkono wa kuume wa Mungu Baba kama tullivyo soma  maandiko .Katika Ukamilifu huo kila goti lita pingwa na kila ulimi uta kiri kuwa Yesu ni Bwana. wafilipi 2.10;11
     Ufunuo wa Yohana 16 ;13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura zikitoka kwa yule joka,na kinywa cha yule mnyama na kinywa cha yule nabii wa uongo.
    Tunaishi katika siku za mwisho sasa na ukweli hatuja jua kikamilifu Nabii wa uongo ni yupi kwa ukamilifu na Mpinga kristo ni yupi kwa sasa lakini kwa kuangalia Dini za mpinga kristo tunazakupata ukweli wenyewe kuwa ni yupi Kadri muda unavyo kwenda tuna zidi kumfahamu
    Katika Dini zampinga Kristo wanamtarajia kama Masiah wao waislamu wanamtarajia Mahdi wa kumi na mbili ,Mabudha wanamtarajia kuja budha wa tano au avatar.
    Waislamu wanaamin kuwa Mahdi atakuwa uzao wa Mohamed na atatanguli kuja kabla ya Yesu Kristo
    na ataleta amani na utulivu duniani katika kipindi cha maovu mengi na vita nyingi duniani na kutakuwa na atakaye tangulia mbele yake kunyosha njia .Kazi kubwa atakayo fanya ni kuua makafir kwa maana wale wote wasiofita imani ya kiislamu watawaua .Inavyosemekana haupo uhakika kuwa Rais wa Iran  Hasan Rouhan ndiye mtangulizi wa Mahdi.
    Wahindu nao wanamin kuwa avatar anakuja na atakuwa mpanda farasi nyeupe na takuwa na upanga mkononi mwake wakiamini mungu wao ni vishnu anayeishi katika nafsi ya mwanadamu.na tatitawala dunia kwa miaka 400000.Na ataleta amani na utulivu duniani.
    Wabudha nao wana amini dunia itakuwa imejaa maovu kiasi ya kwamba atakuja budha anayeitwa Maitreya
    huyu atakuja kuleta amnai na utulivu duniani mtawala wa dunia akiunganisha dunia yote katika utulivu.
    Wayahudi pia wanamtarajia Masiha wao hawa amini kuwa YESU KRISTO pamoja na kuja kupitia wao ni MASIHI.wanamtarajia kuwa ataihidha Himaya ya Utawala wa Daudi.Kujenga Hekalu kuwaunganisha Wayahudi na Kuwashinda adui zake na kuleta amani ya Dunia.
    Free Masoni katika umoja wa Mataifa Muungano wa dini ulianzisha kundi hili la kiimani na lina idara inayoitwa luci Trurt hapo mwanzo lilijulikana kama Lucifer Foundation ndio lililoshinikiza kwa uundwaji wa Umoja wa mataifa.na lina vishirika vya ushirikina kama Freemasons,wicca,mamlaka ya mapambazuko ya dhahabu(Golden dawns)ya nashirikiana kupindua imani Ya Ukristo wa kweli kama vile Honey and Breast Christian Ministry Kanisa lilopo Nairobi Kenya .Na mengine Mengi duniani.
    2wathesalonike 2;8-12 Hapo ndipo atakapofunuliwa  yule asi,ambaye Bwana Yesu atamua kwa pumzi  ya kinywa chake ,na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwepo kwake;9yule ambaye kuja kwake kutakuwa ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani ,kwa uwezo na ishara na ajabu za uongo ;10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanao potea ;kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli,wapate okolewa .11kwa hiyo Mungu anawaletea upotevu,wauamini uongo ;12 ili wahukumiwe wote ambao hawa kuamini kweli,bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
    kutenda kwake Roho hizi chafu zenye sura ya chura ni Ufunuo alioona Yohana katika kisiwa cha patmo hiyo
     Ndugu yangu Mkristo hatkuja mtu kukuambia kuwa mjue kristo kwakuwa sheria ya Mungu ipo katika nia yako hauna anayeweza kukufundisha kumjua Mungu. Waebrania 8;10-12













































































    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPINGA KRISTO HUYU HAPA Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top