JOBLIZ

  • Latest News

    MWONGOZO WA KILIMO CHA BILINGANYA

    KILIMO CHA ZAO LA BILINGANYA

    Historia ya zao la Bilinganya
    Zao hili asili yake ni sehemu za nchi ya India nchi inayo ongoza dunia kwa kilimo cha Bilinganya ni uchina hasa katika pwani za kusini mwa china inayo lima asilima 59% duniani ikifuatiwa na India Uturuki,Misri Irani na Italy.
    Masoko ya zao.
    Zao hili ni zao lililo na masoko ya Nje na ndani kama ilivyo katika utangulizi hulimwa kwa wingi Uchina lakini lina masoko Ulaya na ,Marekani na hata katika masoko ya ndani halina ushindani mkubwa katika masoko ya ndani kama ilivyo mazao ya bustani kama nyanya.
    Matumizi
    Ni zao linalotumika kama mboga au kiungo cha Mboga peke yake au kuchanganywa na mboga zingine
     MAHITAJI YA ZAO KATIKA UZALISHAJI
    Hali ya Hewa
    Zao hili huhitaji haliyahewa ya joto huweza pia kulimwa si chini ya nyuzi 10*c lakini hustawi vizuri katika nyuzi 26*c hadi 29* c
    Udongo
    .Japo zao hili lina mea vizuri kwenye kila aina ya udongo hukuwa na kustawi vema katika udongo tifutifu usio twamisha maji.Udongo ulio katuliwa vizuri huwezesha mizizi kumea vizuri katika  urefu wa mm 600.Hivyo ni mhimu kuliandaa shamba lako vizur kabla ya kupanda
    Miezi mizuri inayoshauriwa katika kilimo hiki ni miezi isiyokuwa na Mvua nyingi kwa kuwa kukiwa na unyenyevu mwingi zao hili huwa halitoi mazao ya kutosha na pia kwenye ukame kusipokuwa na maji ya kutosha huwa halitoi mazao mengi ya kutosha  na Inasemekana kutokana na sifa hizi huwenda ndiyo husababisha kutokuwa na Mafuriko mengi ya zao hili.
    Uoteshaji wa Mbegu
    Mbegu huweza kuoteshwa kwenye vitalu au kupanda moja kwa moja kwenye mashimo na baadae kupinguzia umbali wa 1.8 hadi 2.5 mita mche hadi mche kulingana na rutuba ya udongo miche 10000 huweza kupandwa kwenye ekari moja.
    Masoko;
    Mavuno kwa kila ekari kwa wiki ni takribani viroba 50 kwa wiki ambapo katika Bei iliopo sokoni leo tarehe 30-9-2016 ni shilingi 10000/-kwa viroba 50 ni sawa na 500000/- kwa wiki kwa miezi mitatu hadi sita mfululizo inategemea na utunzaji hasa umwagiliaji.





    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWONGOZO WA KILIMO CHA BILINGANYA Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top