JOBLIZ

  • Latest News

    ONGEZEKO LA MAJESHI YA URUSI MASHARIKI YA KATI YA MSHTUA KATIBU MKUU WA NATO

    Katibu Mkuu wa NATO Bw.Jens Stoltenberg ameshutushwa na ongezo la shughuli za Kijeshi zinazofanywa na Urusi katika Eneo la Kutoka Bahari Ya Baltiki hadi bahari ya Meditrania .Kutokana na Ongezeko hilo NATO imeamua kufanya mazoezi ya kivita katika eneo hilo likishirikisha Askari wa mguu 36000,Manuwari za kivita,60 na Ndege za Kivita za kisasa 160 katika eneo lote la Ureno na Italia.






    Mazoezi haya ya kivita yameanza toka Oktoba 21 na yanatekelezwa na nchi zote 28 zilizowashirika katika umoja wa NATO

    Toka mwaka 1997 mahusiano na Moscow imekuwa ya kirafiki zaidi .Hali hiyo imebadlika toka vita vya Syiria kutokea.Majeshi ya Urusi yamekuwa yakiongezeka Mashariki ya kati na kutishia majeshi ya NATO ambayo hayaungi mkono Utawala Bashir AL Assad.

    Stoltenberg siku ya Alhamis ametoa tahadhari ya ongezeko la majeshi hayo ya Urusi kwa kuwa Majeshi yao yapo Katika maeneo ya kivita ndani ya Syiria yakisaidia Upinzani wa Utawala Wa Bashir Al Assad na wakati huo Urusi ikisaidia kiongozi huyo.

    Oparesheni ya mazoezi yanayoendelea hivi sasa yamepewa jina la TRIDENT JUNCTURE.ikiwa na lengo la kutoa tahadhari kwa majeshi pinzani .

    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ONGEZEKO LA MAJESHI YA URUSI MASHARIKI YA KATI YA MSHTUA KATIBU MKUU WA NATO Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top