JOBLIZ

  • Latest News

    SIFA SABA ZA KIUONGOZI ALIZOONYESHA RAIS MAGUFULI KATIKA UONGOZI WAKE

    Ukiachana na historia ya Utendaji Mzuri akiwa ndani ya Wizara mbalimbali katika Uongozi wa Maraisi wa awamu ya Tatu na ya  nne .Kuna Sifa saba zinazo anza kujitanabaisha katika uongozi wake .
    Kuna  hatua nyingi katika Falsafa  ya Misingi wa Uongozi ambayo  humtanabaisha kiongozi bora.
    Ujenzi wa timu ambayo itaweza kufuata mawazo yako katika utawala na kuwa na mawazo mapya ya kiuongozi.Pia na jinsi ya kuweza kuyatekeleza mawazo hayo mapya katika misingi ya kuweka utawala wenye nguvu .

    1.KUAMINIKA
    Katika siku za mwanzo wa utawala wake amejitahidi sana kujenga IMANI ya kweli kwa wale anao wasimamia kuwa mkweli na mfuatiliaji alizoonyesha katika siku ya kwanza na wiki ya kwanza na mwezi wa kwanza . Alithibitisha hili kwa kuwaaminisha Watanzania kuwa yale aliyokuwa anayasema wakati wa kampeni haikuwa ni porojo za kuvuna kura na kuendelea kujineemesha yeye pamoja na kundi dogo liloko juu lisiloweza kuguswa na yeyote isipokuwa Rais. Na kufumua uozo mkubwa uliokuwepo
    2.UWEZO WA KUKASIMISHA MADARAKA
    Sifa ya usimamizi mkali wa mapato ya Serikali na Utawala kwa ujumla katika kipindi cha jeshi la watu watatu ambalo ilikuwa Yeye Rais,Makamu wa Rais na Katibu Mkuu. Wananchi wali lazimika kukaa karibu na vyombo vya Habari kuiskiliza au kutazama yaliyojiri leo .Na  wananchi wakawa na wasi wasi kuwa jeshi hili litaharibiwa na Mawaziri wake pamoja na Wakuu wa mikoa watakaoteuliwa.Leo hii imekuwa tofauti kauli zilizopo ni kuwa ni heri ukutane na Raisi Magufuli ni balaa ukikutana na Waziri mkuu  na Mawaziri wake.Hii ni sifa ya kipekee .
    3MAWASILIANO NA NCHI ZILIZO JIRANI.
    Rais Magufuli ameonyesha umahiri mkubwa wa mawasiliano ambapo tulikuwa tunelekea kutengwa na nchi zilizokuwa zina tuzunguka Hasa za Afrika Mashariki lakini kwa muda mfupi tu wa nusu mwaka amewezesha kuleta mahusiano mazuri tena makubwa kwa nchi mbili kubwa Uganda na Rwanda ambao walikuwa wametupa mgongo kutokana Ufisadi mkubwa ambao ulikuwa umejitokeza .Mf.Ujenzi wa Reli kutoka Rwanda kwenda Kenya ambapo itatunyima Mapato kutokana Kodi .Kwa kwenda Rwanda na kuondoa vikwazo vya Barabarani Sita vilivyokuwepo.Na pia Kwa Uganda kupitisha bomba la mafuta kwa Gharama nafuu  kupitia Kagera hadi Tanga ambalo litaongeza Pato la Taifa.Kwa hatua hii amewapa moyo majirani zetu na kuyasahau mapungufu yaliyokuwepo ya mawasiliano mabovu.
    4.KUJIAMINI
    Kuahirishwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na kufanya marudio tena Mwezi machi kulikuwa na kila dalili ya kupata vikwazo vya kiuchumi.Pamoja na minongono mingi ya kuwa aingilie kati kusimamisha uchaguzi huo aliweza kutamka wazi kuwa Hata fanya hivyo pamoja na kuwa alitambua atawekewa vikwazo vya kiuchumi .Kwa hatua hii imetanabaisha ni mfuasi mzuri wa Falsafa ya Yai na kifaranga.Ambapo uhai wa kifaranga ailiye ndani ya yai iliaweze kuishi ni lazima ni vunjwe kwa nguvu fulani. Yai likivunjwa kwa nguvu ya nje kifaranga cha ndege mara nyingi lazima kife. Lakini yai likivunjwa kwa nguvu ya kifaranga kukua na kulipasua yai Mara nyingi kifaranga kina ishi.Hii inathibitishwa na kauli yake mwenyewe Magufuli kuwa nchi hii ni Tajiri na ina uwezo wa kujiletea maendeleo yake yenyewe bila kutegemea misaada ya kutoka nje .Na hii ameithibitishia Umma wa  Tanzania kuwa ni kweli ina wezekana baada ya Ofisi nyingi za umma zilikuwa hazipati fedha zake za Utawala awamu hii zimeweza kuzipata na tena kwa wakati.
      5.UWAJIBIKAJI
    Kauli aliyoitoa katika Hotuba yake alipokuwa akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza ilivuta usikivu sana toka mwanzo wake na hadi alipo ikoleza kwa neno amejipa kazi ya kutumbua majibu.Kihalisia serikali au uongozi wa Cheo cha Uraisi ulikuwa umekosa Nguvu ya kiuwajibikaji na kuwajibisha.Hatua ya mwendelezo wa utendaji kazi wake na kushindwa kwenda nje ya Nchi ni kutokana na uchafu na uozo mkubwa alioukuta ndani ya serikali.Amekuwa muwajibikaji mkuu kwa kuhakikisha uozo unatoka na serikali ina kuwa safi.Hii ni wazi ni kiongozi muwajibikaji.
    6.MWENYE MWELEKEO CHANYA
    Mwanafunzi anapokwenda shule huwa tuna tarajia kuwa anakwenda kongezwa Maarifa.Ujuzi na mweleko wa kudumu kwa maisha yake yote.Rais Magufuli ameweza kufumbua macho wengi sio hapa nchini tu lakini hadi nchi za duniani kote kuwa kumbe ina wezekana kuleta Maendeleo kwa nchi unapo kuwa kiongozi imara
    kwa kuyarithisha unayoamini kwa wale unao waongoza na wakakufuata.Dira ya enzi za Nyerere ilikuwa Ujamaa na Kujitegemea na wanachi walifuta huo mwelekeo.Rais Magufuli alifuta sherehe kubwa sana za kitaifa za siku ya Uhuru,na Muungano day akabana fedha za sherehe za kuapiishwa na shughuli nyingi nyingi na fedha hizo akazitumbukiza kwa ajiri ya Maendeleo ya Nchi
    7.MBUNIFU
    Ujenzi wa Barabara mbili ambazo hazikuwa zimetengewa fedha ya mradi wa ujenzi kuweza kupewa fedha kamili na kutekelezwa katika uongozi wake hakuna Rais yeyote ambaye amefanya hivyo kwa muda mfupi hivyo ni mbunifu mahiri mzuri na mtumiaji mzuri wa  uzoefu alioupata wakati akiwa kwenye Wizara ya miundo mbinu na Ujenzi.

    Najua zipo sifa nyingi tu za kuweza kumwelezea Mheshimiwa Rais Magufuli hasa katika kipindi hiki kigumu anapokuwa anaongoza Wanachi waliokwisha kata tamaa na nchi yao. Rais John Jeosph Pombe Magufuli anajitahidi kuonyesha Uzalendo alionao kwa nchi yake.
                                                      MUNGU IBARIKI TANZANI
    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIFA SABA ZA KIUONGOZI ALIZOONYESHA RAIS MAGUFULI KATIKA UONGOZI WAKE Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top