JOBLIZ

  • Latest News

    UGONJWA WA ZIKA NI TISHIO JIPYA DUNIANI

    Watafiti wa Ugonjwa wa Zika wamegundua kuwa Magonjwa ya Ubongo na Uti wa Mgongo yana husiana na dalilia za ugonjwa wa Guillain-Baarre ambao unatokana na virusi vitokanavyo na Mbu
    Magonjwa kama Uti wa Mgongo (Meningitis) Kupooza kutokana na Maambukizo ya Ubongo (Encephalitis na myelits)Watafiti wamegundua kuwa inatokana na maambukizi ya ugonjwa wa Zika.
    Kwa nini ugonjwa huu umekuwa ni tishio kwa muda mfupi.
     Zipo sababu za msingi kwanza ugonjwa huu unaenea katika eneo ambao wapo vijijini mbali na huduma za kiafya .Pia Virus vya ugonjwa vya Zika vimekuwa vikibadilika sana mara kwa mara.
    Mtafiti Dr.Peter Hotez ambaye ni Mwadili katika Chuo cha Bayolar Medicine amesema ugonjwa huu umetokea katika mistu ya Africa.
     Huko Uganda ambapo uligundulika kwa mara ya kwanza Mwaka 1945 hivyo umekuwa ukijibadilisha badilisha hadi ulipofikia sasa.
    Mwaka jana ulionekana tena katika Nchi ya Brazili Bara la Amerika ya Kusini.Na Mwezi Feburari mwaka huu WHO imeutangaza ugonjwa huu kuwa ni janga lingine la kidunia.
    Utafiti uliofanyika kwa vinjiti (aborted fetuses)kumeonekana kuna maabukizo kwenye ubongo wa vinjiti na walipo angalia kwenye konga la uzazi pia lilionyesha maambukizo ambayo huzuia katika makuzi ya mtoto tumboni kwa kuharibu mfumoa wa ufahamu (Central nervous system)
    Madaktari pia wameweza kugnundua pia Virusi vya ugonjwa huu husababisha mabadiliko ya kitabia na uwezo wa kujifunza ambao haukuwepo mwanzoni alipokuwa amezaliwa kabla ya kuugua.
    Ugonjwa huu husababisha udhaifu wa ufanyaji kazi wa misuli ambao husababisha ulemavu wa muda (Temporary paralysis) ambapo wagonjwa huhitaji vifaa vya kupumulia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UGONJWA WA ZIKA NI TISHIO JIPYA DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top