JOBLIZ

  • Latest News

    UGUNDUZI WA GESI YA HELIUM TANZANIA NI GUMZO LA DUNIA

    Gesi ya Helium ni kemikali yenye alama He ni ya pili katika mapangilio jedwali la periodic
    gesi hii haina harufu ,haina rangi wala haina ladha.Hali ya kuganda na kuchemka ni ya chini sana.Hewa hii ni ya pili kwa wepesi yenye tungamo la asilimia 24%
    jina Helium linatokana na miungu ya zamani ya kigriki Mungu wa jua  Helios.Iligunduliwa na Mwana anga wa Ufaransa Jules Janssen mwaka 1868 wakati wa Jua kukamatwa na Mwezi(Solar eclipse)ambapo ilionekana kama mwali wa njano katika tendo la kukamatwa kwa mwezi.
    Gesi hii ni ya muhimu sana kwakuwa inatumika katika shughuli nyingi.Kwakuwa ina hali mdogo sana wa kuganda inatumika katika vifaa vingi Kama vile Katika sumaku za MRI Scannar
    Hutumika viwanda katika vifaa vya kuchomelea kuzui hewa ya oksigeni katika mlipuko,Kutengeneza chengachenga za silicon wafer.Pia hutumika kuinulia maputo makubwa yanayotumika katika usafiri wa anga (Balloon ships)Kwa sababu ya sifa zake hutumika katika utafiti mbalimbali wa kisayansi.
    Kwa asili hewa hii ni nadra sana kupatikana chini ya aridhi na kiasi kikubwa kina patikana angani. Kwa sasa Helium hutenegezwa kwa kuozesha kwa Mionzi (Radioactivty Decay) ya uranium na thoriunm.ambapo hupatikana Kiini cha Helium 4.Upatikanaji mwingine ni kutokana na kunaswa kutoka katika  gesi asilia.
    Wakati madaktari waakionya juu ya matumizi mabaya ya Gesi Helium kuwa kwa sasa ina isha  kwa kuwa ina tumika kujaza maputo kufurahisha watoto na baadae inalipuka hewani na kupotea Mtalaamu wa kudhibiti upumuaji katika chumba cha upasuaji  Anaestheist Tom Dolphin alizuia shughuli hizo kwa kupasua maputo kabla haya jarushwa kwa kitendo hicho ujumbe ulifika vizuri.Na pia mshindi wa Tuzo ya Heshima Robert Richardson alionya kuwa Gesi hii ya Helium itakuwa imekwisha kabisa baada ya miaka 25 hadi 30 na hili angalizo ilikuwa miaka mitano iliyopita .Gharama ya puto dogo ya gesi ya Helium ilkuwa dolla za kimarekani 100 sawa na paundi 64 za Uingereza amabayo ni sawa na shilingi za kitanzania 218574/-Tzshs kwa tarehe ya 5 july 2016.Helium haina Gesi mbadala kwa vifaa vinavyotumia Gesi ya Helium.Kwa umuhimu haiungani na gesi yoyote nyingine ilikuinasa(No Chemical bondage).Sasa Gesi hii imepatikana Tanzania na huu ndio mjadala kwa kuwa kwa makisio yaliyofanyika hifadhi kuu iliyopo sasa katika soko ina kadiriwa kuwa imekwisha ifikapo mwaka 2030 hadi 2040 .Mkakati uliowekwa ni kupiga marufuku kwa puilizaji wa maputo na matumizi mengine yasiyoya muhimu. Mjadala mkuu wa kidunia uliopo sasa kuwa Imepatikana kiasi cha ujazo wa cubic futi 54 bilioni..Vitalu vya Helium vimepatikana kwa kiu ya kupata Gesi asilia na Mbadala wake ikapatikana Helium amabyo inatokana na kuoza kwa mionzi (Redioactivty decay) ambayo imeozeshwa  na joto la kati ya dunia(Earthcore) na kuanza kujipenyeza kuja juu ikanaswa katika mapango chini ya aridhi.Ugunduzi huu umeongozwa na Mtafiti wa miamba ya bonde la ufa  Diveena Danabalan wa chuo cha Durham'.
    Matumizi ya sasa ya Helium ni cubic futi bilioni 8 kwa dunia nzima kutokana hali iliyopo sasa itachukua wastani wa Miaka 7 tu kama ikitolewa yote cubic 54 bilioni toka aridini.
    ANGALIZO KWA WACHUMI NA WATALAMU WA MIKATABA WA TANZANIA SISI TULIROGWA NA NANI HADI TUSIFIKE KWENYE UCHUMI WA KATI.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    1. Casino Restaurants near Foxwoods Resort Casino | Mapyro
      1 제주도 출장안마 Foxwoods Blvd · 2 Foxwoods Blvd · 3 Fairfield St · 4 Pecard 전라북도 출장샵 Rd · 5 광양 출장샵 Pecard Rd · 6 Pecard Rd · 7 Days Inn · 8 Pecard 울산광역 출장안마 Rd. · 9 Days 여주 출장샵 Inn.

      ReplyDelete

    Item Reviewed: UGUNDUZI WA GESI YA HELIUM TANZANIA NI GUMZO LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top