JOBLIZ

  • Latest News

    260 WAMEFARIKI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI ASIA


    Zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo baya zaidi la ardhi, katika kipindi cha muongo mmoja.

    Makundi ya uokoaji yanajikakamua kufikia maeneo ya vijijini zaidi Kaskazini mwa Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan, ilikuwaokoa watu wanodhaniwa kuwa wameathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo hilo hapo jana.
    Kufikia sasa zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo baya zaidi la ardhi, katika kipindi cha muongo mmoja kuwahi kukumba mataifa hayo yaliyoko bara Asia.
    \

    Maafa makubwa zaidi yameripotiwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan.

    Zaidi ya watu elfu mbili wamejeruhiwa.
    Baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Afghanistan, yanadhibitiwa na wanamgambo wa Taliban, na inakuwa vigumu mno kwa maafisa wa serikali na waokoaji kuyafikia ili kutoa usaidizi.
    Maafa makubwa zaidi yameripotiwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan.

    Hali ni mbaya mno katika maeneo yenye milima na mabonde ambako kumeripotiwa maporomoko ya ardhi.

    Vyombo vya dola huko vimeripoti kuwa takriban watu 214 wameaga dunia huko.
    Hali ni mbaya mno katika maeneo yenye milima na mabonde ambako kumeripotiwa maporomoko ya ardhi.
    Kitovu cha tetemeko hilo lenye nguvu ya 7.5 kwenye vipimo vya Richter kilikuwa maeneo yenye milima mingi ya Hindu Kush
    Aidha katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa utawala umetangaza kuwa watu 179 walipoteza maisha yao huku wengine 1,800 wakijeruhiwa.
    Kitovu cha tetemeko hilo lenye nguvu ya 7.5 kwenye vipimo vya Richter kilikuwa maeneo yenye milima mingi ya Hindu Kush, kilomita 45 kusini magharibi mwa Jarm, Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani imesema.

    • Blogger Comments
    • Facebook Commentshttps://www.facebook.com/groups/kallyboy/

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: 260 WAMEFARIKI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI ASIA Rating: 5 Reviewed By: ndalahwabohe
    Scroll to Top