Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameunda majimbo 28 ikiwa ni zawadi ya kusherehekea sikukuu ya Krismas kati ya majimbo 10 yaliyokuwa hapo mwanzo.
Ambapo wajuzi wa mambo ya kisiasa wanasema hayataleta chachu ya mkataba wa amani nchini Sudani ya Kusini.Magavana kumi waliokuwepo wameteuliwa pamoja na wengine 21 kuongoza majimbo hayo.
Uamuzi wa Rais Kiir umetokana na wapiganaji pinzani wa Msituni 150 kurejea toka Msituni hadi Mji mkuu wa Juba ikiwa ni mojawapo wa makubaliano wa kushirikiana katika maswala ya Utawala pamoja na makundi megine ya upinzani wa kisiasa.
Uamuzi huo sio wa kikatiba kwa kuwa sio maamuzi yaliyo katika Bunge au Rais mwenye uwezo wa kuunda majimbo mapya .Hivyo Uamuzi huo umepingwa vikali na Msemaji wa kambi ya upinzani Bw James Gatdet Dak kwa kuwa ugawaji wa majimbo huo umetokana ukabila kwa kuwa kila kabila limepewa jimbo lake.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza kupiganwa toka Desemba 2013Mamia kwa Maalfu ya raia wameshapoteza uhai wao na watu takribani milioni mbili wamehama makazi yao na kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao.

0 comments:
Post a Comment